Maelezo kuhusu Tukio la Usalama wa Data la 2016

Mnamo Oktoba 2016, Uber ilikumbwa na tukio la kiusalama lililosababisha uvujaji wa taarifa za akaunti za wasafiri na madereva.

Taarifa ya madereva ilijumuisha majina, anwani za barua pepe na namba za simu za akaunti kwa jumla. Pamoja na hayo, namba za leseni za takribani madereva 600,000 wa Marekani zilipakuliwa. Wataalamu wetu wa kufanya uchunguzi hawajapata ushahidi wowote unaoonesha kwamba maelezo ya historia ya maeneo ya safari, namba za kadi za benki, namba za akaunti za benki, namba za ustawi wa jamii au tarehe za kuzaliwa zilidukuliwa.



Tukio hili lilipotokea, tulichukua hatua mara moja ili kulinda data, tukazuia ufikiaji wowote zaidi usioidhinishwa na tukaimarisha ulinzi wetu wa data.



Tunawajulisha madereva walioathirika moja kwa moja kupitia barua au barua pepe na tunafuatilia vocha zao na kuwapa ulinzi dhidi ya udukuzi wowote bila malipo.



Tulipogundua tukio hilo Novemba 2016, tulichukua hatua za kusitisha na kuzuia madhara, lakini hatukuwajulisha madereva. Tunaamini kwamba tukio hili lilikuwa kosa na ndiyo maana tumechukua hatua stahiki kuzuia hali kama hiyo tena. Hatujapata ushahidi wowote wa ulaghai au udanganyifu unaohusiana na tukio hili.