Tuko hapa kukusaidia

Kubadilisha Maelezo ya Akaunti

Unaweza kutumia App ya Dereva kubadilisha namba yako ya simu, barua pepe na mtaa unakoishi kwa kufuata hatua zifuatazo:

1. Fungua App kisha ubonyeze picha yako iliyo katika kona ya upande wa juu kulia
2. Bonyeza "Akaunti", kisha ubonyeze "Badilisha akaunti"
3. Chagua maelezo unayotaka kubadilisha kisha uweke maelezo mapya
4. Tutakuomba uweke namba ya kuthibitisha au nenosiri lako la sasa ili kuthibitisha mabadiliko yako

KUTHIBITISHA MABADILIKO KWENYE AKAUNTI

- Namba ya simu: utapokea namba ya kuthibitisha kupitia SMS. Weka namba uliyopokea kwenye App ili uthibitishe mabadiliko hayo.

- Barua pepe (iOS pekee): tutakutumia namba ya kuthibitisha kwenye anwani yako mpya ya barua pepe. Weka namba uliyopokea kwenye App ili uthibitishe mabadiliko hayo. Tutakutumia pia arifa ya barua pepe kwenye anwani yako ya awali. Usipopokea barua pepe, angalia folda ya barua taka na maendelezo ya anwani ya barua pepe yako kabla ya kuomba namba nyingine. Ikiwa bado hupokei namba ya kuthibitisha, bonyeza "Nina tatizo".

- Nenosiri: utaulizwa uweke nenosiri jipya kwenye App. Manenosiri yanapaswa kuwa na angalau herufi 5.
Sign in to get help