Kujisajili kwa kutumia kuponi ya mwaliko

Ukurasa wa kujisajili kwenye Uber hukuruhusu uweke kuponi ya mwaliko kutoka kwa rafiki yako ili uweze kupokea zawadi ya mwaliko. Sera, masharti na viwango vya pesa vinavyohusiana na mialiko hutofautiana kati ya miji.

Unapojisajili moja kwa moja kutokana na mwaliko wa barua pepe au SMS, kuponi ya mwaliko wa rafiki yako hutumika kiotomatiki. Bofya kiungo kilicho kwenye mwaliko ili ujisajili.