Kukubali safari ndefu

Wakati mwingine, unaweza kupokea ombi la usafiri kuelekea mahali mbali zaidi na mahali ulipo sasa. Utaona ujumbe wa "Safari ndefu" ukiwa na makadirio ya muda katika sehemu ya chini ya skrini yako unapotumiwa maombi kama hayo.

Ukipokea ombi la usafiri unaokutaka kwenda mbali zaidi ya unavyotaka, usikubali. Ombi hilo litatumwa kiotomatiki kwa dereva mwingine aliye karibu. Ikiwa umekubali ombi kimakosa, tafadhali ghairi safari hiyo.

KUMBUKA: Kuna safari zinazoweza kumalizika kiotomatiki baada ya saa kadhaa. Utajulishwa kabla ya safari kumalizika, msafiri uliye naye anaweza kuitisha usafiri mwingine ikiwa angependa kuendelea. Tunakushauri umjulishe msafiri kwamba safari itaisha mara utakapopokea moja ya arifa hizi.