Tuko hapa kukusaidia

Kutumia App nyingine au kupokea simu ukiwa mtandaoni

Ukiingia mtandaoni lakini ubadilishe na kuanza kutumia App nyingine kabla ya kupokea ombi la msafiri, huenda ukapokea arifa inayoibuka kila baada ya dakika 3 kukukumbusha uondoke mtandaoni ikiwa hutaki kupokea maombi ya wasafiri. Unapoendelea na safari, App yako haitakutumia arifa zinazoibuka.

App yako ya Dereva wa Uber huendelea kufanya kazi unapotumia App nyingine kwenye simu. Maelezo ya GPS huendelea kukusanywa ili kuhakikisha kwamba tunarekodi nauli sahihi za safari zako.

Fuata sheria za eneo ulipo zinazohusu utumiaji wa simu. Tafadhali kumbuka kwamba kutumia simu unapoendesha gari kunaweza kukuchanganya na ni hatari. Wasafiri wengine pia huona kuwa umewakosea adabu na unahatarisha maisha yao.
Sign in to get help