Tuko hapa kukusaidia

Kuwaalika madereva na wasafiri

Kila mtu aliye na akaunti ya Uber ana kuponi anayoweza kutumia kuwaalika marafiki ambao wangependa kufungua akaunti ya msafiri au ya dereva. Utapokea zawadi wakati:

- Wasafiri wapya wataweka kuponi yako ya mwaliko kabla ya kuitisha safari yao ya kwanza
- Madereva wapya hujisajili kwa kutumia kuponi ya mwaliko kisha kukamilisha idadi fulani ya safari au masharti mengine

Unaweza tu kutumia zawadi moja ya mwaliko. Ikiwa dereva uliyemwalika amejisajili kuendesha gari au kusafirisha bidhaa awali, huenda usipokee zawadi.

Mbinu za kupata na kutuma kuponi ya mwaliko:

- Bonyeza "Alika Marafiki Sasa" katika kichupo cha Mapato katika App yako. Utaona msimbo wako wa mwaliko kwenye sehemu ya chini ya skrini yako. Unaweza pia kuona orodha ya madereva uliowaalika, hali yao ya mwaliko, na zawadi utakayopokea wakisafiri kwa mara ya kwanza au kukamilisha idadi ya safari zinazotakiwa.

2. Chagua "Mialiko" kwenye menyu kuu katika partners.uber.com. Unaweza kupata maelezo hayo hapa ambayo ni sawa na yale utapata kwenye App ya dereva.

3. Ikiwa unatumia app ya msafiri, chagua Safari Bila Malipo kwenye menyu ya App ili ukague kuponi yako ya mwaliko na uwaalike marafiki.

Mwaliko wako ukikubaliwa, utaarifiwa kupitia barua pepe au ndani ya App. Zawadi yako inaweza kupatikana kwenye sehemu ya "Malipo na Mambo Mengine" ya taarifa yako ya malipo baada ya wiki moja au mbili.

Ikiwa hujapokea malipo ya kumwalika msafiri, huenda msafiri huyo hakuweka kuponi yako wakati wa kujisajili au hajasafiri kwa mara ya kwanza. Uko huru kumkumbusha au kumhimiza afanye hivyo!

Tafadhali kumbuka kwamba akaunti yako ya udereva haionyeshi idadi yote ya mialiko yako iliyokubaliwa. Hutaweza kubadilisha kuponi yako ya mwaliko. Ingawa baadhi ya watu unaowaalika watapokea zawadi kwa kujisajili kwa kutumia kuponi yako, hawataona kiasi wanachoweza kupokea.
Sign in to get help