Tuko hapa kukusaidia

Ni data gani inapatikana katika dashibodi yangu ya mshirika?

Angalia na udhibiti maelezo ya akaunti ya udereva kwenye Dashibodi ya Mshirika. Angalia historia ya safari, taarifa za malipo na hati za dereva.
TAARIFA ZA MALIPO

Kichupo cha Taarifa za Malipo kinakuwezesha kufikia taarifa zako kulingana na kipindi cha malipo. Kila taarifa ya malipo inajumuisha maelezo yafuatayo:

- Jumla ya mapato kutoka kwenye safari na ofa
- Mapato ya kila siku na historia ya safari. Kila tarehe inajumuisha orodha ya kina ya safari zote za siku husika, ikiwamo wakati wa kuchukuliwa, gari, muda, umbali, jumla ya mapato ya safari husika

Ili kupakua taarifa yako ya malipo na muhtasari wa historia ya safari, fuata hatua hizi:

1. Bonyeza "Chapisha taarifa" kwenye sehemu ya chini ya ukurasa ili ufungue hati unayoweza kuchapisha
2. Kulingana na kivinjari unachotumia, unaweza ukatumia menyu ya kivinjari ili uchapishe hati hii
3. Hifadhi nakala ya PDF ya ukurasa huu ili uweke rekodi zako

Muhtasari wa shughuli za dereva (ikijumuisha jumla ya safari ulizokamilisha, saa ulizotumia mtandaoni, kiwango cha kukubali safari, na matukio ya kughairi safari) kwa kipindi cha malipo cha taarifa kinaoneshwa kwenye ukurasa wa wavuti.

Ingawa taarifa hii haijajumuishwa katika toleo la taarifa unayoweza kuchapisha, unaweza kuchapisha mwenyewe ukurasa wa wavuti kwenye menyu ya kivinjari chako na uihifadhi kama PDF.

MAELEZO YA SAFARI
Bofya safari husika ili upate maelezo ya kina ya safari. Hatua hii itafungua kichupo kipya kinachojumuisha maelezo yafuatayo:

- Maelezo ya kina ya nauli kulingana na kipengele, ikiwamo kiasi cha pesa alizolipa msafiri, na kiasi ambacho Uber ilipokea kutokana nayo
- Muda wa safari na umbali uliosafiri
- Gari lililotumika kwa safari hii na namba pleti yake

Ili upakue maelezo ya safari ya mtu binafsi, fungua kidirisha cha kuchapisha na uhifadhi ukurasa kama PDF.

HATI ZA KODI
Ili uangalie na kupakua hati zako za kodi, nenda kwenye kichupo cha "Maelezo kuhusu kodi". Uber itakutumia muhtasari wa kila mwaka ili upakue PDF au uchapishe kwa ajili ya rekodi zako.

MAELEZO YA BENKI
Kichupo cha "Benki" kina maelezo ya akaunti yako na kadi ya benki. Kwa usalama wa malipo yako, maelezo nyeti (kama vile namba kamili ya akaunti ya benki) yanafichwa.

HATI ZA DEREVA
Hati nyinginezo za dereva hazipatikani kwa ukamilifu kwenye tovuti. Katika kichupo cha "Dhibiti hati zako", unaweza kuthibitisha hati ulizopakia kwenye tovuti. Hati hizi zinaweza kujumuisha leseni yako ya udereva na usajili wa gari, bima, na fomu za ukaguzi.

Kwa sababu una uwezo wa kufikia hati zako binafsi, Uber haitatoa nakala za hati ulizopakia, ili kulinda usalama wa maelezo yako.
Sign in to get help