Nifanye nini ikiwa bidhaa ninayosafirisha itaghairiwa?

Ikiwa agizo ulilokubali limeghairiwa, utapokea arifa ibukizi katika programu yako ya dereva. Tupa mahali salama chakula ambacho kimeghairiwa. Ikiwa uko njiani kuelekea eneo la kupeleka chakula kisha agizo lighairiwe, bado utalipwa ada ya kuchukua chakula. Utaona malipo haya kwenye sehemu ya "HISTORIA YA SAFARI" katika programu.