Tuko hapa kukusaidia

Nimetatizika kupakua App kwenye Android

Ikiwa unatumia simu ya Android, unaweza kupakua App kwa kutafuta "Dereva wa Uber" kwenye Google Play Store. Ikiwa unapata tatizo la kupakua App ya Dereva wa Uber kwenye simu yako ya Android na kifaa chako kinakuonyesha ujumbe wa hitilafu unaosema "imeshindwa kupata muunganisho wa seva salama", jaribu kufunga kivinjari kwa kubofya menyu ya kifaa chako na kutelezesha kidole kwenda kulia huku umeshikilia App ya kivinjari.

Pia unaweza kufuta vidakuzi vilivyo kwenye kivinjari chako. Kufanya hivyo, bonyeza menyu iliyo katika kivinjari, (kwa kawaida ni aikoni ya vistari vitatu katika kona ya kulia kwenye skrini ya kifaa) kisha chagua Mipangilio > Faragha na Usalama halafu bonyeza "Futa Vidakuzi". Tafadhali kumbuka kwamba kufanya hivyo kutafuta manenosiri yoyote uliyohifadhi pamoja na data ya kuvinjari.

Ikiwa bado unatatizika kupakua App, tafadhali tujulishe hapa.
Sign in to get help