3 - Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia Programu ya Dereva

Jinsi programu ya Dereva inavyofanya kazi:

Kuingia mtandaoni

Programu ya Dereva inapatikana wakati wowote. Kwa hivyo, wakati wowote unapokuwa tayari kuendesha gari, fungua programu kisha ubofye NENDA.

Kukubali maombi ya safari

Ukiwa mtandaoni, utaanza kupokea maombi ya safari kutoka kwa Wasafiri katika eneo lako kiotomatiki. Simu yako itatoa sauti ya arifa na utapewa safari inayoonyesha kiasi cha mapato mapema. Bofya ili ukubali au ubofye alama ya mkasi kwenye sehemu ya juu kulia ili ukatae.

Maelekezo ya hatua kwa hatua

Programu hii inafanya iwe rahisi kumpata mteja wako na kuelekea mahali anakoenda kwa kutumia maelekezo ya hatua kwa hatua. Unaweza pia kuchagua kutumia mfumo wa uelekezaji wa kampuni nyingine ikiwa unapendelea.

Mapato kwa kila safari

Angalia kiasi ulichojipatia baada ya kila safari na ufuatilie hatua unazopiga ili utimize malengo ya mapato yako ya kila siku na kila wiki. Mapato hutumwa kiotomatiki kwenye akaunti yako ya benki kila wiki.

Usipitwe na lolote

Pata ujumbe kuhusu kila kitu kuanzia matukio yanayokaribia na fursa za kujipatia mapato hadi taarifa kuhusu akaunti yako na vipengele vipya. Kila unapopokea ujumbe mpya, beji itaonekana kwenye picha yako katika kona ya juu kulia kwenye skrini ya ramani yako. Bofya ili uusome.

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia programu

Iwe ni safari yako ya kwanza au ya 100, una nyenzo iliyojaa vidokezi na video zenye taarifa muhimu. Bofya picha yako katika sehemu ya juu kulia ya skrini ya ramani yako. Kisha bofya Msaada juu ya Akaunti.

Fuatilia mapato yako

Fuatilia kwa urahisi hatua unazopiga ili kutimiza malengo yako ya mapato ya kila siku na kila wiki. Unaweza pia kufikia muhtasari wa mapato yako kwa kubofya mara moja tu. Bofya ikoni ya nauli kwenye skrini ya ramani yako, kisha utelezeshe kulia na kushoto ili uchunguze mapato yako.

Baada ya kuifahamu programu ya Dereva wa Uber, fahamu kuhusu mapato unayoweza kujipatia: