Unapotumia Uber, unatuamini na data zako binafsi. Tumejizatiti kudumisha uaminifu huo, na yote huanza kwa kukusaidia kuelewa taratibu zetu za faragha.
Angalizo hili linamhusu nani?
Angalizo hili linahusu:
- Watumiaji wa huduma za Uber duniani kote. Hii ni pamoja na:
- Wasafiri
- Madereva
- Yeyote anayeitumia Uber Eats au huduma zinazohusiana na Uber
- Yeyote anayewasiliana na Uber au kutoa taarifa kwa Uber, isipokuwa kama ilivyoelezwa katika Angalizo la Faragha
Nini kiko katika Angalizo la Faragha?
Angalizo la Faragha la Uber lina maelezo kuhusu:
- Ukusanyaji wa taarifa: aina za data ambazo Uber hukusanya unapotumia huduma zetu
- Matumizi ya taarifa: jinsi Uber inavyotumia taarifa zilizokusanywa
- Kushirikiana kwa taarifa: masharti ambayo Uber hushirikiana data na wahusika wengine
- Chaguo zako: haki na chaguo zako kuhusu taarifa unazotoa kwa Uber
Kwa kuelewa kikamilifu taratibu za Uber, tafadhali pitia Angalizo la Faragha kwa undani.