NI lazima msafiri awe na umri wa angalau miaka 18 ili awe na akaunti ya Uber na aweze kuita gari. Yeyote aliye na umri wa chini ya miaka 18 anapaswa aandamane na mtu aliye na umri wa miaka 18 au zaidi katika safari yoyote.
Ikiwa wewe ni dereva katika mji usioruhusu watoto kuita gari, unapaswa kukataa ombi lolote la usafiri kutoka kwa mtu unayeamini kwamba hajafikisha umri wa miaka 18. Wakati wa kuchukua msafiri, ikiwa unadhani kwamba hajafikisha umri unaoruhusiwa, unaweza kumuuliza akuoneshe leseni yake ya udereva au kitambulisho ili uthibitishe. Ikiwa msafiri hajafikisha umri wa miaka inayotakiwa, tafadhali usianzishe safari au kumruhusu asafiri nawe.