Kwa nini kuna tofauti katika kadirio na jumla la salio langu?

Ikiwa umeingia katika akaunti au unatumia programu yako ya dereva, unaweza kuangalia makadirio ya malipo yako kabla ya mwisho wa mzunguko wa kila wiki unayoedelea na upokee jumla ya malipo. Makadirio ya malipo utakayopokea huhesabiwa kwa kujumlisha mapato ya nauli katika wiki inayoendelea.

Tafadhali kumbuka kwamba kiasi hicho huenda hakitajumuisha malipo ya ziada ambayo unaweza kupokea, yakiwemo malipo ya ofa, zawadi za kuwaalika wengine au mapato uliyohakikishiwa. Malipo hayo ya ziada huhesabiwa mwishoni mwa kipindi kinachoendelea cha malipo ya kila wiki.