Kwa nini baadhi ya maeneo yaliyo kwenye ramani yamepakwa rangi tofauti?

Ramani iliyo kwenye App yako hupaka sehemu fulani za mji rangi za manjano, machungwa na nyekundu. Rangi hizi huashiria maeneo yaliyo na wasafiri wengi.

Jinufaishe kwa maelezo haya kwa kuelekea kwenye maeneo ambako nauli imeongezwa ili upokee maombi ya usafiri kutoka huko. Wasafiri wanaoitisha usafiri katika maeneo yaliyo na rangi hizi wamekubali kulipa nauli ya juu.

Unaweza kukuza ukubwa wa maeneo yaliyopakwa rangi kwenye ramani ili uone vizidisho vya nauli vikiwa vimeoneshwa kama namba. Kwa mfano, unaweza kuona maeneo yaliyo na rangi ambayo yana vizidisho vya nauli vya 1.3x, 1.5x au 2.2x.