Tuko hapa kukusaidia

Kuchangia gharama ya nauli na rafiki

Ukiwa safarini, mgawanyiko wa nauli unakuwezesha kugawanya nauli ya safari kwa usawa kati ya wasafiri. Ili kugawanya nauli:

1. Tuma ombi la safari.
2. Chagua Mgawanyo wa nauli chini ya kioo cha simu yako.
3. Ingiza majina au namba za simu za wasafiri.

Kama unatumia programu mpya:
1. Tuma ombi la safari
2. Futa kioo cha simu yako kuanzia chini kuelekea juu na gusa njia ya malipo uliyochagua.
3. Gusa mgawanyiko wa nauli.
4. Ingiza majina namba za simu za abiria wengine.

Kila uliyemualika atatumiwa ujumbe wa kumtaka akubali mgawanyiko wa nauli yako. Kisha nauli ya safari yako itagawanywa sawa sawa kwa wasafiri waliyokubali pamoja na wewe.

Tafadhali zingatia kuwa kila mshiriki atakatwa kiasi kidogo ($0.25) ili kugawanya nauli.

Kama msafiri akichagua kutokukubali mgawanyiko wa nauli au hana mfumo halali wa malipo, utatakiwa kulipia sehemu yako ya nauli pamoja na ya wote waliokataa kukubali kilipa. Promosheni ulizopewa na Uber zitatumika kwenye sehemu ya malipo uliyotakiwa kulipa wewe tu.

Uwezo wa kugawanya nauli haupatikani kwenye uchaguzi wa huduma za magari aina zote, kwa mfano UberPOOL. Tafadhali zingatia kuwa hatuwezi kugawanya nauli baada ya kukamilisha safari.