Uber hutumiaje anwani za mawasiliano?

Kuanzia Mei 2018, programu ya Uber haitatumika tena kuunganisha anwani za simu yako kwenye akaunti yako. Kipengele hiki cha hiari kiliruhusu programu ya Uber ikupe mapendekezo ya kibinafsi (kama vile kupendekeza marafiki wa kualika). Anwani kutoka kwa simu yako hazitasawazishwa tena kwa seva za Uber, na maelezo ya anwani yaliyosawazishwa hapo awali yatafutwa.

Programu itaendelea kuomba ruhusa ya anwani ikiwa unatumia vipengele vinavyoonyesha kitabu chako cha anwani ndani ya programu, kwa mfano:

  • Anwani Unaoaminika
  • Gawanya Nauli
  • Shiriki ETA
  • Alika Rafiki

Uber itaendelea kuhifadhi taarifa za watu mahususi unaowachagua unapotumia vipengele hivyo, kama vile marafiki unaogawa nao nauli.