Kumkadiria dereva

Ukadiriaji hutuwezesha kuhakikisha uzoefu mzuri kwa msafiri na dereva, kwa hivyo tunayachukulia kwa uzito. Madereva wenye ukadiriaji wa chini wanaweza kupoteza ufikiaji wa programu.

Ili kumkadiria dereva, fuata maelekezo katika programu mwishoni mwa safari. Pia utaombwa kumkadiria dereva wako kutoka chini ya stakabadhi uliyoipokea kwa barua pepe.

Kama utamkadiria dereva:

  • Nyota 5, utaona chaguo la kumpa pongezi. Wasafiri wengi hutoa ukadiriaji wa nyota 5 isipokuwa kulikuwa na tatizo maalum na safari.
  • Chini ya nyota 5, utaombwa kutoa maoni maalum kuhusu safari au dereva kutoka kwenye orodha ya matatizo ya kawaida. Ukadiriaji wa nyota 1 kawaida una maana kulikuwa na tatizo kubwa na dereva.

Matatizo kama bei ya safari, matatizo ya programu, au kukutanisha kusikofaa za pool si kosa la dereva, hivyo hayatahesabiwa kwenye ukadiriaji wao wa jumla.

Unaweza kumkadiria dereva ndani ya siku 30 baada ya safari. Dereva hatawahi kuona ukadiriaji uliompa.