Jinsi ya kutumia memo ya gharama

Wasimamizi wa akaunti ya Uber for Business ya kazini wanaweza kuhitaji misimbo ya gharama kwa safari zinazofanywa kwenye wasifu wa kazini.

Kama msimamizi wako alihitaji misimbo ya gharama, utaombwa kuchagua msimbo wa gharama kutoka kwenye orodha au kuingiza yako mwenyewe kabla ya kuomba safari.

Kama hutaombwi lakini unataka kuingiza msimbo wa gharama au memo, unaweza kufanya hivyo kwenye kichupo cha Maelezo ya gharama kilicho chini ya skrini yako baada ya kuomba safari.

Kumbuka: Memo ya gharama lazima ijazwe kabla ya safari kumalizika. Huwezi kuhariri maelezo ya gharama baada ya safari kukamilika.

Misimbo ya gharama zitaonyeshwa kwenye taarifa yako ya kila mwezi na stakabadhi za safari. Wasimamizi wa kampuni yako pia wanaweza kuona taarifa hii kwenye Dashibodi yao. Muulize msimamizi wako kuhusu sera ya memo ya gharama ya kampuni yako.