Tuko hapa kukusaidia

Kupakua App ya msafiri (iOS)

Unaweza kupakua na kuweka App ya msafiri wa Uber kwenye simu zilizo na toleo la iOS 8 na mpya zaidi. Fungua App Store kwenye simu yako, kisha ufuate hatua zilizo hapa chini.

1. Bonyeza "Tafuta" kwenye upau wa menyu chini, kisha uandike "Uber" kwenye upau wa kutafutia
2. Chagua "Uber" kwenye matokeo ya utafutaji
3. Kando ya aikoni ya Uber, bonyeza "Pata." Huenda ukatakiwa kuweka nenosiri au Apple ID.
4. Ukishapakua App, hali ya "Pata" itabadilika kuwa "Fungua." Bonyeza "Fungua" ili ufungue App.
6. Ukiwa umefungua App ya Uber, bonyeza "Ingia kwenye akaunti" ikiwa una akaunti au "Jisajili" ili ufungue akaunti mpya