ETA hufanyaje kazi?

Kabla ya safari kuanza, programu yako itakuonyesha makadirio ya muda ambao dereva atatumia kufika eneo la kukupakia.

Baada ya safari kuanza, programu yako itakuonyesha makadirio ya muda utakaotumia kufika eneo unaloelekea.

Tafadhali zingatia kuwa makadirio ya safari siyo uhakika. Sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wa dereva kama foleni kubwa au ukarabati wa barabara zinaweza kuathiri muda wa safari.

Kabla ya kutuma ombi la safari, programu yako itakuonyesha muda. Unaweza kuona muda kwenye boksi jeusi lenye neno WEKA ENEO LA KUPAKIWA. Muda huu ni wa makadirio juu ya muda atakaotumia dereva aliye karibu na wewe kufika eneo ulilochagua kupakiwa/kuanza safari yako.

Kwa kutumia kisogezeo chini ya kioo cha simu yako, unaweza kuona makadirio ya muda wa kuwasili kwa kila chaguo la huduma ya gari inayopatikana ndani ya jiji lako.

Baada ya kuanza safari, programu yako itakukumbusha mara kwa mara juu ya makadirio ya muda utakaotumia kufika eneo unaloelekea.