Wasiliana na dereva wako kwa kutumia TalkBack

Chaguzi za kupiga simu au kutuma ujumbe kwa dereva wako zinaonekana kwenye upau mweupe chini ya skrini yako mara tu unapopangwa.

Kuna ikoni ya simu na kisanduku cha kuingiza ujumbe kwenye upau mweupe ambapo jina la dereva na taarifa za gari zinaonekana.

Kupigia dereva wako simu:

  1. Gusa mara moja, kisha gusa mara mbili ikoni ya mduara ya simu chini ya taarifa za dereva wako
  2. Gusa mara moja, kisha gusa mara mbili nambari ya simu au kitufe cha "FREE CALL"
  3. Simu yako itampigia dereva wako moja kwa moja kulingana na chaguo ulilochagua

Kumtumia ujumbe dereva wako:

  1. Gusa mara moja, kisha gusa mara mbili sehemu ya maandishi chini ya taarifa za dereva wako
  2. Andika au sema ujumbe wako
  3. Gusa mara moja, kisha gusa mara mbili kitufe cha "SEND"