Tuko hapa kukusaidia

Itisha usafiri kwa kutumia TalkBack

Fuata utaratibu huu kuitisha usafiri wakati umewasha TalkBack:

1. Bonyeza mara moja, kisha ubonyeze mara mbili kisanduku kilichoandikwa "Ungependa kwenda wapi?" Weka mahali unakoenda au chagua kwenye orodha ya maeneo yanayopendekezwa.

2. Eneo lako la kuchukuliwa huwekwa kiotomatiki kuwa mahali ulipo kwa mujibu wa GPS. Ili kulibadilisha, bonyeza eneo lako la kuchukuliwa, kisha uguse mara mbili ili kubadilisha mahali ulipo.

3. Tumia vidole viwili kukagua aina ya magari yanayopatikana mahali ulipo. Bonyeza mara moja, kisha ubonyeze mara mbili ili uchague aina ya usafiri unaotaka.

4. Bonyeza mara moja, kisha ubonyeze mara mbili kitufe kilichoandikwa "THIBITISHA KUCHUKULIWA" kilicho sehemu ya chini ya skrini ya kuitisha usafiri

5. Utapokea arifa dereva wako atakapowasili. Ujumbe huo utasomwa kwa sauti.

6. Bonyeza mara moja, kisha ubonyeze mara mbili kitufe kilicho sehemu ya chini ya skrini yako ili uweze kufungua chaguo zifuatazo:

- Kuwasiliana na dereva wako - bonyeza mara moja, kisha ubonyeze mara mbili aikoni ya mviringo ya simu ili upige simu kwa namba ya dereva wako au upige simu bila malipo

- Kughairi safari - bonyeza mara moja, kisha ubonyeze mara mbili kitufe cha "Ghairi", bonyeza mara moja, kisha ubonyeze mara mbili kitufe cha "Ndiyo, ghairi" ili kuthibitisha.

- Kuonesha mahali ulipo - Bonyeza mara moja, kisha ubonyeze mara mbili kitufe cha "Onesha Mahali", halafu uchague watu kwenye orodha ya anwani zako. Uber huwatumia watu unaowachagua kiungo ili waweze kufuatilia safari yako.

- Kuchangia nauli - bonyeza mara moja, kisha ubonyeze mara mbili kitufe cha "Changia Nauli" halafu uchague jina la mtu