Tuko hapa kukusaidia

Kuchangia gharama ya nauli na rafiki

Wakati wa safari, kipengele cha Kuchangia Nauli hukuruhusu kcuhangua nauli ya safari kwa usawa kati wa wasafiri. Ili ujichange:

.Ita gari.
2. Chagua Changia Nauli kwenye sehemu ya chini ya skrini yako.
3. Andika majina au namba za simu za wasafiri wengine.

Kama unatumia programu mpya:
1. Ita gari.
2. Telezesha kidole juu kutoka sehemu ya chini ya programu na ugonge mbinu yako ya malipo uliyochagua.
3. Gonga Changia Nauli
4. Weka majina au namba za simu za wasafiri wengine.

Kila mtu unayemwalika ataarifiwa kuhusu gari uliloita ili akubali kujichanga. Nauli ya safari inachangwa kwa usawa kati yako na wasafiri wanaokubali.

Kumbuka kwamba wakati wa kuchangia nauli, kila msafiri hutozwa ada ya senti 25 ya kutumia huduma. Risiti yako itaonyesha jumla ya ada ya kuchangia nauli iliyolipwa na wasafiri wote

Msafiri akiamua kutokubali kuchangia nauli au ikiwa hana mbinu ya malipo inayofanya kazi, basi utatozwa kiasi chako na chake. Ofa zinazotumika kwenye akaunti yako zianatumika tu kwa sehemu yako ya nauli.

Huenda huduma ya kuchangia nauli isipatikane kwa huduma zote za Uber Kumbuka kwamba hatuwezi kuchangia nauli safari ikikamilika.

Kumbuka: Huenda Apple Pay isitumike katika kuchangia nauli Ikiwa unatumia Apple Pay lakini unataka kuchangia nauli, huenda ukahitaji kutumia mbinu nyingine ya malipo. Unaweza kubadilisha ili utumie Apple Pay kwenye safari yako itakayofuata.