Tuko hapa kukusaidia

Kupakua App ya msafiri

HATUA ZA KUPAKUA KWENYE ANDROID

Unaweza kupakua na kusakinisha programu ya wasafiri ya Uber kwenye simu za Android zilizo na mfumo wa uendeshaji wa 4.0.3 na matoleo mapya zaidi. Nenda kwenye duka la Google Play na ufuate hatua hizi:

1. Gusa aikoni ya Google Play.
2. Gusa aikoni ya utafutaji, andika Uber kisha uguse Tafuta.
3. Chagua aikoni ya Uber kisha uguse SAKINISHA.
4. Baada ya kukamilisha kuweka App, bonyeza FUNGUA.
5. Ukiwa umefungua App ya Uber, gusa INGIA ikiwa una akaunti au uguse JISAJILI ili ufungue akaunti.
WINDOWS

Kuanzia Juni 2018, App ya Uber haitapatikana tena kwenye simu za Windows. Watumiaji wa Windows wanaweza kuagiza safari kupitia m.uber.com.