Tuko hapa kukusaidia

Maelezo kuhusu Tukio la Kiusalama wa Data la 2016

Mwezi Oktoba 2016, Uber ilikumbwa na tukio la kiusalama lililosababisha kuvuja kwa maelezo ya akaunti za wasafiri na madereva.Maelezo ya akaunti yaliyovuja kote ulimwenguni yalikuwa majina, anwani za barua pepe na namba za simu za wasafiri. Wataalamu wetu makandarasi wa uchunguzi hawajapata ushahidi wowote kwamba maelezo kuhusu historia ya mahali, namba za kadi za benki, namba za akaunti za benki, namba za Ustawi wa Jamii au tarehe za kuzaliwa zilifichuliwa.

Tukio hili lilipotokea, tulichukua hatua za mara moja kulinda data, kufunga ufikiaji wowote zaidi usioidhinishwa na kuimarisha ulinzi wetu wa data.

JE, NINATAKIWA KUCHUKUA HATUA YOYOTE?
Tunaamini kwamba hakuna msafiri anatakiwa kuchukua hatua yoyote. Hatujapata ushahidi wowote wa ulaghai au udanganyifu unaohusiana na tukio hili. Tunafuatilia akaunti zilizoathiriwa na tumeziainisha ili zlindwe zaidi dhidi ya ulaghai.