Kiungo changu cha kubadilisha nenosiri hakifunguki

Unapowasiliana nasi ili kubadilisha nenosiri la akaunti yako ya Uber, unafaa kupokea barua pepe baada ya dakika chache. Barua pepe hiyo itakuwa na kiungo kitakachokusaidia kubadilisha nenosiri lako.

Kwa sababu za usalama, muda wa kutumia kiungo hicho utakwisha baada ya dakika 10. Fungua kiungo hicho haraka iwezekanavyo au usubiri hadi uwe tayari kwa mchakato wa kubadilisha nenosiri kabla ya kuomba kulibadilisha.

Endapo kiungo chako cha kubadilisha nenosiri hakifanyi kazi, tafadhali anza upya katika uber.com/forgot-password. Hakikisha kwamba anwani yako ya barua pepe ni sahihi, kisha ufungue kiungo kitakachotumwa kupitia barua pepe nyingine utakayopokea ya kubadilisha nenosiri.

Ikiwa umeshindwa kubadilisha nenosiri lako au kufungua akaunti yako, tafadhali wasiliana nasi hapa chini.

Ujumbe wa kiotomatiki utatumwa hapa ili kuthibitisha kwamba hakika ni wewe. Tafadhali fungua ujumbe huo na uchague "Thibitisha anwani ya barua pepe" ili uunganishwe na mwanatimu wetu. Writing in from