Nimepokea ujumbe unaoniambia kwamba kuna mtu ameniitishia usafiri wa Uber. Hii ina maana gani?

Ikiwa umepokea ujumbe unaosema kwamba gari lako la Uber linakuja, kuna mtu ambaye amekuratibia usafiri. Fuata maelezo yaliyo kwenye ujumbe ili ukubali usafiri na uone maelezo ya kuchukuliwa.

Ikiwa umepokea ujumbe ulio na kiungo cha kuitisha usafiri wa Uber, hii ina maana kwamba biashara imekuitishia usafiri unaoweza kuutumia wakati wowote katika siku uliyopanga (kabla ya saa 6 usiku). Bonyeza kiungo kilicho katika ujumbe ukiwa tayari kuitisha usafiri.

Ikiwa hutaki kupokea tena safari au kama unataka kuacha kupokea ujumbe, jibu kwa neno STOP.