Tuko hapa kukusaidia

Pitia menyu kwa kutumia TalkBack

Ili menyu ya programu ya Uber itumie TalkBack, fungua programu yako kisha ubonyeze sehemu ya juu kushoto mwa skrini yako mara mbili ili ufungue menyu. Chagua zifuatazo zinaonekana kuanzia juu hadi chini:

Safari zako - Sehemu inaorodhesha safari ulizokamilisha, au unaweza kuona safari zinazofuata, ulizoratibiwa. Tumia vidole viwili kupitia kwenye historia ya safari zako. Chagua moja ili kupata usaidizi katika safari, kuwasilisha maoni au kuona stakabadhi ya safari.

Malipo - katika sehemu hii unaweza kuongeza au kubadilisha mbinu ya malipo

Usaidizi kwa wateja - soma makala tofauti ili upate majibu ya maswali yako kuhusu Uber. Unaweza pia kuwasilisha maoni kuhusu vipengele vya ufikivu katika sehemu hii

Safari bila malipo - tumia kuponi ya mwaliko wa kibinafsi iliyohifadhiwa kwenye sehemu hii ili kuwaalika watu wengine watumie Uber

Mipangilio - weka maelezo yako ya anwani, weka maeneo unayosafiri sana kama vile nyumbani au kazini au uongeze anwani ili uweze kuonesha mahali ulipo kwa urahisi kabla au safari inapoendelea

WASILIANA NA HUDUMA YA USAIDIZI KWA WATEJA

Ikiwa una maswali au maoni yanayohusiana na ufikivu, unaweza kuyawasilisha kwenye sehemu ya Usaidizi kwa wateja katika kichupo cha Menyu. Ripoti tatizo jingine lolote linalohusiana na safari kwa kuchagua safari mahususi kwenye sehemu ya "Safari Zako" katika menyu. Kwenye skrini inayotokea, unaweza kuchagua hoja mbalimbali ili uweze kuripoti tatizo.