Tuko hapa kukusaidia

Pitia menyu kwa kutumia VoiceOver

Ili kutumia menyu ya programu ya Uber kupitia VoiceOver, fungua programu yako kisha ubonyeze mara mbili sehemu ya juu kushoto kwenye skrini yako ili ufungue menyu. Chagua zifuatazo zinaonekana kuanzia juu hadi chini:

Safari zako - sehemu hii inaorodhesha safari ulizokamilisha, au unaweza kuona safari zinazofuata, ulizoratibiwa. Telezesha vidole vitatu kwenye sehemu ya historia yako ya safari. Chagua moja ili kupata usaidizi katika safari, kuwasilisha maoni au kuona stakabadhi ya safari.

Malipo - katika sehemu hii unaweza kuongeza au kubadilisha njia ya malipo

Usaidizi kwa wateja - soma makala tofauti ili upate majibu ya maswali yako kuhusu Uber. Unaweza pia kuwasilisha maoni kuhusu vipengele vya ufikivu katika sehemu hii.

Safari bila malipo - tumia kuponi ya mwaliko wa kibinafsi iliyohifadhiwa kwenye sehemu hii ili kuwaalika watu wengine watumie Uber

Mipangilio - weka maelezo yako ya anwani, weka maeneo unayosafiri sana kama vile nyumbani au kazini au uongeze anwani ili uweze kushiriki eneo lako kwa urahisi kabla au safari inapoendelea

WASILIANA NA HUDUMA YA USAIDIZI KWA WATEJA

Ikiwa una maswali au maoni yanayohusiana na ufikivu, unaweza kuwasiliana nasi kwa kubonyeza sehemu ya "Ufikivu" katika sehemu ya "Usaidizi kwa wateja" kwenye menyu. Ripoti suala jingine lolote linalohusiana na safari kwa kuchagua safari mahususi kwenye sehemu ya "Safari Zako" katika menyu. Kwenye skrini inayotokea, unaweza kuchagua hoja mbalimbali ili uweze kuripoti tatizo.