Itisha usafiri kwa kutumia TalkBack

Hapa ni jinsi ya kuomba safari ukiwa na TalkBack imewashwa:

  1. Gusa mara moja, kisha gusa mara mbili kwenye kisanduku cha “Where to?”. Ingiza mahali unakoenda, au chagua kutoka kwenye orodha ya mahali unakoenda yaliyopendekezwa.
  2. Eneo la kuchukulia msafiri huwekwa moja kwa moja kwa kutumia eneo lako la GPS. Ili kubadilisha, gusa eneo la kuchukulia msafiri, kisha gusa mara mbili ili kuhariri eneo lako.
  3. Tumia vidole viwili kuvinjari chaguzi za gari zinazopatikana katika eneo lako. Gusa mara moja, kisha gusa mara mbili kuchagua moja kwa ajili ya safari yako.
  4. Gusa mara moja, kisha gusa mara mbili kitufe cha “CONFIRM PICKUP” kilicho chini ya skrini yako kuomba safari yako.
  5. Utapokea taarifa wakati dereva wako atakapofika. Ujumbe utaelezwa kwa sauti.
  6. Gusa mara moja, kisha gusa mara mbili upau ulioko chini ya skrini yako kufikia chaguzi zifuatazo:
  • Wasiliana na dereva wako - Gusa mara moja, kisha gusa mara mbili ikoni ya simu mviringo kupiga nambari ya simu ya dereva wako au kupiga simu bure
  • Ghairi safari yako - Gusa mara moja, kisha gusa mara mbili kitufe cha “Cancel”, kisha gusa mara moja, kisha gusa mara mbili kitufe cha “Yes, cancel” kuthibitisha.
  • Shiriki hali yako - Gusa mara moja, kisha gusa mara mbili kitufe cha “Share Status”, kisha chagua watu kutoka kwenye orodha yako ya anwani. Uber itatuma ujumbe wa maandishi kwa anwani hao ili kufuatilia safari yako.
  • Changia nauli - Gusa mara moja, kisha gusa mara mbili kitufe cha “Split Fare” na chagua anwani