Utaona ombi lililodokezwa na kifaa chako la ruhusa ya kushiriki maelezo ya eneo lako unapojiandikisha kwa Uber, ambayo ni pamoja na data ya eneo iliyokusanywa kupitia Bluetooth na mawimbi ya karibu ya wifi. Kwa huduma bora zaidi inayopatikana, programu kwa chaguomsingi hukuomba uwashe huduma za eneo "huku ukitumia programu" kwa kutumia "mahali mahususi."
Tunatumia data ya eneo ili:
- Kutafuta madereva walioko karibu nawe na uwasaidie kuelekea kwenye eneo lako la kuchukuliwa
- Kuonyesha historia ya safari katika stakabadhi zako
- Kuelewa na kusuluhisha kesi za usaidizi
- Kutatua na kurekebisha hitilafu za programu
Chaguo za mipangilio ya eneo
Kwa vifaa vya iOS
- Kila wakati: Tunaweza kukusanya maelezo ya eneo wakati wowote, hata wakati hutumii programu ya Uber. Ikiwa huduma inahitaji Kila wakati, tutaomba ruhusa yako utakapowasha huduma.
- Unapotumia Programu: Tunaweza kukusanya maelezo ya eneo wakati programu inaonekana kwenye skrini yako au wakati umeomba safari na wakati wa safari yako. Utapata arifa iOS kwenye skrini ikiwa maelezo ya mahali yanakusanywa chinichini ukiweka mipangilio ya Unapotumia.
- Usiwahi: Chaguo hili huzima huduma za mahali kwenye programu ya Uber. Bado unaweza kutumia programu, lakini itakubidi uweke mwenyewe eneo la kuchukuliwa na la kushushwa. Maelezo ya mahali ulipo yatakusanywa kutoka kwa dereva wakati wa safari na yataunganishwa kwenye akaunti yako, hata kama umezima huduma za mahali kwenye programu yako.
- Eneo Mahususi: Chaguo hili huzima huduma za mahali mahususi kwenye programu ya Uber. Ikiwa imezimwa, bado unaweza kutumia programu, lakini itakubidi uweke mwenyewe eneo la kuchukuliwa na la kushukishwa. Maelezo ya eneo mahususi yatakusanywa kutoka kwa dereva wakati wa safari na yataunganishwa kwenye akaunti yako, hata kama umezima huduma za eneo mahususi kwenye programu yako.
Kwa Simu za Android
- Unapotumia Programu: Tunaweza kukusanya maelezo ya eneo wakati programu inaonekana kwenye skrini yako au wakati umeomba safari na wakati wa safari yako. Utapata arifa kwenye skrini ikiwa maelezo ya mahali yanakusanywa katika mandhari ya nyuma ukiweka mipangilio ya Unapotumia.
- Wakati huu tu: Chaguo hili huwezesha huduma za eneo kwa programu ya Uber kwa tukio hili pekee. Ukichagua chaguo hili, utadokezwa tena ruhusa za eneo wakati mwingine utakapotumia programu ya Uber.
- Usiruhusu: Chaguo hili huzima huduma za mahali kwenye programu ya Uber. Bado unaweza kutumia programu, lakini itakubidi uweke mwenyewe eneo la kuchukuliwa na la kushushwa. Maelezo ya mahali ulipo yatakusanywa kutoka kwa dereva wakati wa safari na yataunganishwa kwenye akaunti yako, hata kama umezima huduma za mahali kwenye programu yako.
- Eneo Linalokadiriwa: Chaguo hili huzima huduma za mahali mahususi kwenye programu ya Uber. Inapoteuliwa, bado unaweza kutumia programu, lakini itakubidi uweke mwenyewe eneo la kuchukuliwa na la kushushwa. Maelezo ya Eneo Linalokadiriwa yatakusanywa kutoka kwa dereva wakati wa safari na yataunganishwa kwenye akaunti yako, hata kama umezima huduma za mahali kwenye programu yako.
Unaweza kudhibiti mipangilio ya eneo lako wakati wowote katika mapendeleo ya eneo la kifaa chako chini ya programu ya Uber.
Kuonesha miji na serikali
Katika hali fulani, tunatakiwa kuyapa mamlaka ya miji, serikali na za usafiri, taarifa kuhusu safari zinazofanywa kwa kutumia huduma zetu.
Ili kutimiza masharti haya, huwa tunakusanya data ya mahali na muhuri wa muda kutoka kwenye magari yaliyo katika mfumo wetu.
Data hii huipa miji taarifa kuhusu mahali ambapo kila oda inaanza, inasimama na barabara iliyotumiwa. Kati ya data yote ya oda tunayotoa kwa miji, hamna tunayokusanya kutoka kwenye simu yako ya mkononi wala hamna data inayoweza kukutambulisha, hata hivyo data ya safari inaweza kuhusishwa na wewe, ikifuatiliwa. Katika hali kama hizi, tutakujulisha kabla ya safari.
Kuna matukio maalum, kama kuzuia ulaghai na kukabiliana na matukio ya usalama, ambapo Uber inaweza kukusanya maelezo ya mahali alipo msafiri katika mandhari ya nyuma, akiweka mipangilio ya “Unapotumia”. Katika hali kama hii, utapata arifa.
Uber hutumia maelezo ya mahali ulipo kwa mujibu wa Ilani ya Faragha ya Mtumiaji.