Tuko hapa kukusaidia

Wasiliana na dereva wako kwa kutumia TalkBack

Chaguo la kumpigia simu au kumwandikia ujumbe dereva litaonekana katika upau mweupe, sehemu ya chini ya skrini yako mkishakutanishwa.

Kuna aikoni ya simu na kisanduku cha kuandika ujumbe katika upau mweupe palipo na jina la dereva na maelezo ya gari.

Ili umpigie dereva wako simu:

1. Bonyeza mara moja, kisha ubonyeze mara mbili aikoni ya mviringo ya simu iliyo chini ya taarifa ya dereva wako
2. Bonyeza mara moja, kisha ubonyeze mara mbili namba ya simu au kitufe cha "PIGA SIMU BILA MALIPO"
3. Simu yako itampigia dereva kiotomatiki kutegemea chaguo utakaloteua

Ili umtumie dereva wako ujumbe:

1. Bonyeza mara moja, kisha ubonyeze mara mbili sehemu ya kuandika ujumbe iliyo chini ya taarifa ya dereva wako
2. Andika au tamka ujumbe wako
3. Bonyeza mara moja, kisha ubonyeze mara mbili kitufe cha "TUMA"