Ninaweza kuona salio langu wapi?

Unaweza kuangalia salio lako la Uber kwa kuchagua "Malipo" kwenye menyu. Salio lako huonyeshwa katika sarafu ya kadi yako ya mikopo. Tafdhali kumbuka, salio la Uber haliwezi kubadilishwa kutoka sarafu moja kuwa nyingine.

Salio la Uber litatumiwa kiotomatiki kama chaguo la kwanza la kulipia safari yako ijayo. Kabla au wakati umeanza safari, unaweza kuchagua mbinu ambayo ungependa kutumia kulipa na uwezeshe au kuzima chaguo la salio la Uber.

Unapofika mwisho wa safari yako, mbinu ya malipo uliyochagua itatozwa. Ikiwa ulizima chaguo la salio la Uber, basi njia ya malipo uliyoweka itatozwa nauli kamili. Ikiwa chaguo la salio la Uber limewashwa lakini lina kiasi kisichoweza kulipa nauli yako kwa ukamilifu, kiasi kinachobaki kitatozwa mbinu ya malipo iliyo kwenye akaunti yako.

Ikiwa una safari ya bila malipo, itatumika kiotomatiki katika safari yako ijayo. Chaguo la safari za bila malipo haliwezi kuzimwa.