Mbona nimetozwa kwa chakula ambacho sijapokea?

Mshirika anayesafirisha chakula anapowasili mahali anapopeleka chakula, hujaribu kuwasiliana na mteja. Programu ya Uber Eats pia humwarifu mteja kuhusu majaribio ya kuwasiliana naye. Mshirika anayesafirisha chakula pia husubiri kwa muda fulani akifika katika eneo la kupeleka chakula.

Ikiwa Mshirika anayesafirisha chakula hawezi kusafirisha chakula kutokana na jambo hili, programu ya Uber Eats hutuma arifa kuhusu jaribio la kusafirisha chakula ambalo halijakamilishwa. Majaribio haya yote ya mawasiliano yataonekana katika programu ya Uber Eats.

Ikiwa Mshirika anayesafirisha chakula hataweza kufikisha chakula chako kutokana na hali hii, utatozwa kwa kuagiza.