Ghairi agizo langu

Unaweza kughairi agizo katika programu ya Uber Eats.

ILI KUGHAIRI AGIZO LAKO:
1. Bonyeza aikoni ya stakabadhi katika upau wa menyu ya chini
2. Chagua ulichoagiza
3. Katika skrini ya ulichoagiza, bofya "GHAIRI AGIZO"
4. Utaoneshwa arifa ibukizi ili uthibitishe hatua yako, bofya "GHAIRI AGIZO" tena
5. Baada ya kuthibitisha, chagua sababu ya kughairi, kisha bofya "NIMEMALIZA"

KUMBUKA: Ukighairi chakula ulichoagiza BAADA ya mgahawa kuanza kukiandaa, huenda utapokea kiasi fulani cha pesa unazopaswa kurejeshewa.