Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu mpango wa mapendekezo

Ni nani anayeweza kushiriki katika mpango wa mapendekezo?

Wateja wote wa Uber for Business wa Marekani wanaotimiza masharti ya ustahiki wanaweza kushiriki katika mpango wa mapendekezo. Kwa kupendekeza Uber for Business kwa marafiki na wafanyakazi wenzako, unaweza kupata hadi $500 za kutumia kwa safari za binafsi, oda za chakula na usafirishaji kupitia Uber na Uber Eats.

Watu unaowapendekeza ambao wanatimiza masharti ya ustahiki pia wanaweza kupata zawadi baada ya shirika lao kufungua akaunti ya Uber for Business na kutumia $100 ndani ya siku 60 za kwanza.

Je, masharti ya ustahiki ni yapi?

Mtu anayempendekeza sharti awe sehemu ya shirika la Uber for Business lililoko Marekani na awasilishe pendekezo kabla ya tarehe ya mwisho ya ofa.

Mtu anayependekezwa lazima atumie kiungo cha pendekezo kilichotumwa na Uber ili kufungua akaunti mpya ya U4B ya Marekani na atumie angalau $100 kwenye akaunti yake ndani ya siku 60 tangu ilipofunguliwa.

Ninaweza kuwasilisha vipi pendekezo?

Ili kuwasilisha pendekezo:

  1. Ingia kwenye dashibodi yako ya Uber for Business.
  2. Chagua wasifu wa akaunti yako kwenye menyu. Utaona kitufe cha kushiriki katika mpango wa mapendekezo. Fomu ya pendekezo inakuwezesha kuweka maelezo ya mawasiliano ya rafiki au shirika unalopendekezea Uber for Business.
  3. Jaza fomu ya pendekezo na tutakutumia kiungo na maelekezo ya kujisajili kwenye anwani ya barua pepe uliyotupa.

Ni nani ninayeweza kupendekeza kwenye mpango wa mapendekezo?

Unaweza kumpendekeza mtu yeyote, mradi afungue akaunti ya U4B ya Marekani. Zawadi za mapendekezo zinatolewa kwa USD.

Ninaweza kupata pesa ngapi?

Unaweza kupata vocha ya $50 kwa hadi mapendekezo 10 katika kipindi cha miezi 3—hiyo ni jumla ya vocha za Uber za hadi $500 ambazo unaweza kutumia katika safari na usafirishaji wa binafsi.

Nitapokea zawadi zangu lini na vipi?

Unastahiki kupata zawadi baada ya shirika kufungua akaunti mpya ya Uber for Business kwa kutumia kiungo cha pendekezo ulichoweka na ikiwa shirika linatimiza masharti ya ustahiki.

Wewe na mtu uliyempendekeza mtapokea vocha ya Uber ya $50 kupitia barua pepe ya kutumia katika safari za kibinafsi au kusafirisha bidhaa katika programu za Uber au Uber Eats mwishoni mwa mwezi unaofuata.

Baada ya kupokea vocha yako, unaweza kufuata hatua hizi ili utumie:

  1. Ingia katika programu ya Uber au fungua akaunti ya Uber katika uber.com.
  2. Bofya kiungo kilicho katika barua pepe yako ili utumie vocha.
  3. Vocha itawekwa kiotomatiki kwenye akaunti yako na itatumiwa kwenye safari au oda yako ijayo inayostahiki.

Je, una maswali? Pata maelezo zaidi kuhusu vocha za biashara.

Je, ninaweza kufuatilia hali ya mapendekezo yangu?

Kwa sasa hatutoi huduma za ufuatiliaji wa mapendekezo. Hata hivyo, tutakuarifu kupitia barua pepe ya akaunti yako ya Uber for Business pindi pendekezo lako litakapotimiza vigezo vya kupata zawadi. Unaweza kuwasiliana na business-support@uber.com wakati wowote ikiwa unahitaji usaidizi zaidi.

Je, ninaweza kupendekeza wateja katika nchi yoyote?

Ni mashirika nchini Marekani pekee yanayoweza kushiriki katika mpango huu kwa wakati huu.

Mimi au mtu niliyempendekeza hakupokea zawadi ya pendekezo. Ninapaswa kufanya nini?

Unastahiki kupata zawadi baada ya shirika unalopendekeza kutimiza masharti ya kustahiki.

Zawadi hutumwa kupitia barua pepe mwezi unaofuata baada ya kustahiki. Ikiwa hujapata arifa ya zawadi yako kwenye kikasha cha barua pepe iliyosajiliwa na Uber for Business, tafadhali wasiliana na business-support@uber.com.

Mtu niliyempendekeza hakujisajili kwa kutumia mwaliko wa barua pepe niliyomtumia. Ninaweza kupokea vipi vocha ya pendekezo?

Utaweza kupata zawadi, mradi tu uliyempendekeza ajisajili kwenye akaunti kwa kutumia kiungo kilicho kwenye mwaliko wa barua pepe. Si lazima atumie anwani ya barua pepe iliyopokea mwaliko wa kujisajili kwa Uber for Business.

Ikiwa mtu uliyempendekeza atapokea mapendekezo kutoka kwa watumaji wengi, mtumaji wa kwanza ndiye tu atakayepata zawadi.

Mtu mwingine isipokuwa mtu niliyempendekeza amefungua akaunti ya Uber for Business. Je, sote tutapata zawadi?

Ikiwa mtu unayempendekeza atasambaza barua pepe kwa mtu mwingine ili akamilishe mchakato wa kujisajili, bado unastahiki kupokea zawadi ikiwa ni mshirika wa shirika hilo hilo la Marekani na anatumia kiungo cha pendekezo kilicho kwenye mwaliko wa barua pepe. Anwani uliyoweka tu ndiyo itakayopokea zawadi ya unayempendekeza, si mtu aliyemsambazia kiungo.

Je, ninaweza kupokea zawadi za wateja wa awali niliowapendekeza kabla ya mpango wa mapendekezo kuanza?

Hapana. Mpango wa mapendekezo hufuatilia mapendekezo ya wateja wapya wa Uber for Business. Hatuwezi kutoa zawadi kwa wateja waliojisajili kabla ya mpango huo kuzinduliwa.